The Revolutionary Government of Zanzibar
Zanzibar Planning Commission

#

KIKAO CHA KUJADILI MWENENDO WA MFUMKO WA BEI ZANZIBAR

Tume ya Mipango Zanzibar kupitia idara ya Ukuzaji Uchumi imefanya kikao na wadau mbali mbali ili kujadili kuhusu mwenendo wa Mfumko wa bei Zanzibar. Kikao hicho kilichoongozwa na Katibu Mtendaji Dkt. Rahma S. Mahfoudh kimefanyika katika ukumbi wa Tume ya Mipango Vuga Mjini Zanzibar.

10 September, 2022 Read More
#

KIKAO CHA KUJADILI MPANGO WA UTEKELEZAJI WA AJENDA YA UTAFITI YA MWAKA 2021-2026

Tume ya Mipango Zanzibar kupitia idara ya Utafiti imefanya kikao na wadau mbali mbali ili kujadili kuhusu Mpango wa Utekelezaji wa Ajenda ya Utafiti ya mwaka 2021-2026 kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo Cha Sayansi na Teknolojia Karume Zanzibar.

02 September, 2022 Read More
#

KIKAO CHA KAMATI YA WATAALAMU YA MKURABITA

Katibu mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dr. Juma Malik Akil akifungua kikao cha kamati ya uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za wanyonge Tanzania (MKURABITA) Kilichojadili Utekelezaji wa mwaka 2021/2022 na mwelekeo 2022/2023.

08 July, 2022 Read More
#

UZINDUZI WA UTOAJI HATI ZA URASIMISHAJI ARDHI

Tume ya Mipango Zanzibar kupitia idara ya mipango ya kitaifa, maendeleo ya kisekta na kupunguza umasikini, imeshiriki katika Uzinduzi wa utoaji hati za urasimishaji ardhi kwa wananchi wa shehia ya Shakani ambapo wananchi mbali mbali walikamilisha taratibu zote wamepatiwa Hati za ardhi zao.

10 May, 2021 Read More
#

KIKAO CHA WADAU WA UNFPA

Tume ya Mipango Zanzibar Kupitia Idara ya mipango na maendeleo ya watendakazi imefanya kikao kazi cha wadau wa UNFPA kujadili utekelezaji na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa programu mbali mbali katika kipindi cha robo mwaka Machi hadi Juni 2022. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Tume ya Mipango na kimeongozwa na Kamishna wa Idara hiyo Ndugu Salama Ramadhan Makame.

5 July, 2022 Read More
#

MAANDALIZI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA KUPAMBANA NA UMASIKINI ZANZIBAR

Tume ya Mipango Zanzibar Kupitia Idara ya mipango ya kitaifa, maendeleo ya kisekta na kupunguza umasikini imefanya kikao cha pamoja na wadau kutoka taasisi mbali mbali kujadili maandalizi ya Maadhimisho ya wiki ya kupambana na umasikini Zanzibar inayotarajiwa kuadhimishwa kuanzia tarehe 13 hadi 17 October 2022.

29 June,2022 Read More
#

MAFUNZO YA MKURABITA NA ZADEP KWA MAAFISA WA OFISI YA RAIS, FEDHA NA MIPANGO ZANZIBAR

Tume ya Mipango Zanzibar Kupitia Idara ya mipango ya kitaifa, maendeleo ya kisekta na kupunguza umasikini imefanya mafunzo ya kutoa uelewa juu ya mradi wa MKURABITA kwa maafisa na watendaji mbali mbali wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango.

23 June, 2022 Read More
#

MAANDALIZI YA UTEKELEZAJI WA RIPOTI YA HIARI KWA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs)

Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar Dkt. Rahma S. Mahfoudh amefungua kikao kazi cha siku 5 cha maandalizi ya Utekelezaji wa Ripoti ya Hiari kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa upande wa Zanzibar mwaka 2023 kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar.

22 June, 2022 Read More