THE REVOLUTIONARY GOVERNMENT OF ZANZIBAR
ZANZIBAR PLANNING COMMISSION

#

KIKAO CHA KUJADILI HALI YA MFUMKO WA BEI ZANZIBAR.


2023-02-05

Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar, Dkt. Rahma S. Mahfoudh akiongoza kikao cha kujadili mfumko wa bei na mwenendo wa bei za bidhaa kwa mwezi wa Januari mwaka 2023. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Tume ya Mipango, kilihudhuriwa na washiriki kutoka Taasisi mbali mbali za Serikali, walipata fursa ya kutoa maoni, mapendekezo ili kuweza kuondoa changamoto zilizopo kuhusu mfumko wa bei za bidhaa.