KIKAO CHA UHAMASISHAJI KUTOA MAONI DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 .
2023-07-26
MKOA WA MJINI MAGHARIBI
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana Mustafa amesema Ushiriki wa Wadau na Wananchi katika utoaji wa Maoni ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 ni hatua moja ya kupatikana kwa Dira ambayo itakidhi haja na Mahitaji muhim ya Taifa
Akifungua semina ya uelemishaji umma kwa ngazi ya Mkoa juu ya Matayarisho ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 katika Afisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Vuga amesema ili kuwafikia Dira hiyo ni vyema kwa Viongozi hao kuwa Mabalozi kwa Wananchi kwa kuwaelemisha umuhim wa kutoa Elimu na Dira yenye manufaa kwa Watanzania wote.
Amesema lengo lengo la kushiriki Viongozi na Wananchi katika Dira ya 2050 ni kuondosha kasoro zilizopo katika Maeneo mbali mbali ya Kiuchumi na Kijamii .
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema uwajinikaji wa viongozi wa ngazi za Mkoa kufika kwa Wananchi kuwapatia Elimu na kufika Dira shirikishi kwa kupata maoni ya Watanzania
Kwa Upande wake Mjumbe wa Kamati kuu Kupitia Dira 2050 Moza R. Omar amesema mchakato wa utayarishaji wa Dira 2050 Dira hiyo itaweza kutoa nafasi kwa Wananchi kutoa maoni yao ambayo yatafanyiwa kazi na kufikia Dira waitakayo .
Nao washiriki wa semina hiyo wamesema Dira ijayo Iweze kugusa maeneo muhimu ikiwemo Elimu ya Ufundi ili pindi wanapomaliza masomo yao waweze kujiajiri.