KIKAO CHA UHAMASISHAJI DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 TANZANIA.
2023-07-25
MKOA WA KUSINI UNGUJA
mkuu wa mkoa wa kusini unguja hadidi rashid hadid amesema utolewaji wa elimu kwa viongozi wa serikali tàasisi binafsi na viongozi wa dini na makundi ya vijana kutawajengea uelewa ili waweze kuwaelimisha wananchii umuhimu wa dira ya maendeleo kwa maskahi ya wananchi nà taifa kwa ujumla kwa kutoa maoni muda unakapofika.
akifungua mkutano wa uelimishaji umma katika maandalizi ya dira ya taifa ya maendeleo 2050 kwa viongozi wa mkoa , kidini na vijana katika mkoa wa kusini tunguu amesema viongozi hao wanawajibu wa kuwa mstari wa mbele kwa kuitambua dira na kutoa maoni yao.
àmesma ushiriki wa wadau utaweza kupata dira jumuilishi yenye kukidhi mahitaji stahiki ya taifa katika kipindi cha miaka 25 ijayo.
akiwasilisha mada ya uhamasishaji wa ushiriki wa wadau katika maandalizi ya dira ya taifa ya maendeleo ya 2050 moza radhani omar ambae ni mjumbe wa kamati kuu ya kupitia dira ya 2050 amesema zoezi litakapo halitomuacha mtu kwani wataweza kutoa maoni yao kwa dira wanayoitaka kuelewa majukumu yao ili kufanikisha lengo la dira kwa maendeleo ya taifa.
wakitoa maoni yao washiriki wa mkutano huo wameombà dira ya 2050 iweze kuzingatia maeneo muhimu ikama vile mazingira ili yaweze kuleta dira kwa kizazi cha baadae.