KIKAO CHA KAMATI YA WATAALAMU YA MKURABITA
2023-02-10
Kamishna, Idara ya Mipango Kitaifa, Maendeleo ya Kisekta na Kupunguza Umaskini Nd. Mohammed Salim masoud, ameongoza kikao cha kamati ya Wataalamu cha kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji ya shughuli za MKURABITA katika kipindi cha July-Disemba 2022/2023.Katika kikao hicho, Mratibu wa MKURABITA kwa upande wa Zanzibar amewasilisha Mwelekeo na Makadirio ya Matumizi ya Shughuli za MKURABITA kwa mwaka 2023/2024 pamoja na Kujadili Utekelezeji wa Maagizo ya Waziri wa nchi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Jenista Mhagama alipotembelea Miradi ya MKURABITA kwa upande wa Zanzibar.Kwa upande wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Zanzibar wamewasilisha taarifa ya kamisheni ya utekelezaji wa kazi za Utambuzi wa Ardhi kwa kipindi cha Julai hadi Disemba 2022 kwa Unguja na Pemba Ambapo maeneo walio yafanyia utambuzi huo ni Jambiani kwa upande wa Unguja na Gombani kwa PembaKwa Unguja wameweza kufanya kazi ya Upimaji wa Viwanja,uwekaji wa mipaka na utoaji wa ramani ya maeneo husika pamoja na ujazaji wa fomu za utambuzi wa ardhi hayo yalifanyika kwa sambamba na baada hapo uhakiki wa fomu na kuingiza taarifa ukafata baadae ambapo maeneo 350 yalitambulika.Kwa upande wa Pemba walianza na kuwapa elimu kwa wananchi wanao ishi maeneo ya Gombani na vitongoji vyake kama vile Korea, Madina, judo, Mperani, Chukwani, Miburani na Gombani ya kati.Kazi ya upimaji, utoaji ramani,pamoja na ujazwaji wa fomu za utambuzi zilifanyika ambapo maeneo 537 yamefanyiwa upimaji .Wizara ya biashara maendeleo ya viwanda nao kwa upande wao wameweza kukamilisha ujenzi wa kituo jumuishi kilichopo wilaya ya chake chake Pemba na kuweza kufatilia utekelezaji wa majukumu katika kituo Jumuishi kilichopo Darajani Wilaya ya Mjini na Mkokotoni Baraza la Mji kaskazini A.Kituo Jumuishi cha Darajani ni kituo ambacho kinatoa huduma tofauti tofauti kama vile Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali (BPRA),Baraza la Manispa la Mjini, ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali ,wakala wa chakula dawa na vipodozi Zanzibar ( ZFDA)Vile vile Kituo cha Jumuishi cha Urasimishaji cha Kaskazini A Kimeweza kuwatambuwa wafanyabiashara wadogo wadogo 311 na kuwapa uwelewa wa usajili wa biashara, kutoa leseni za biashara 983 kwa wafanyabiashara waliokuepo kwenye Mkoa wa Kaskazini A pamoja na wafanyabiashara 24 kusajiliwa katika mfumo wa usajili wa biashara na mali (BPRA) na vikundi 36 vimetambuliwa na kupewa maelekezo ya mahitaji ya kukamilisha usajili wao.